Na
Tallib Ussi Hamad
Wakati
Dunia ikiendelea kupiga hatua zaidi kushirikisha vijana wengie katika nafasi
mbali mbali za uongozi inaelezwa kuwa visiwani Zanzibar hali ya ushiriki wa
vijana katika nafasi za maamuzi bado haijaridhisha.
Kulingana na matakwa ya Umoja wa Mataifa unamtafsiri
kijana ni mtu aliye baina ya umri wa miaka 15 na
24. Na, kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar, kijana ni mtu
mwenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35. Kulingana na sensa ya watu na makaazi ya
mwaka 2012, Zanzibar ina idadi ya watu 1,303,569 ambapo kati yake wanawake ni
672,892 sawa 51 na wanaume ni 630,677 sawa na 49. Katika idadi hiyo, vijana
walikadiriwa kufikia 456,249 ambao ni sawa na 35%. Miongoni mwao vijana wa kike
ni 232,687.
Katika
mkutano wa hivi karibuni ulioitishwa na TAMWA-ZNZ na kuwashirikisha wadau mbali
mbali vijana wa vyama vya siasa na wasomi wa vyuo vikuu ulibaini uwepo wa
mazingira yasiokua rafiki kwa vijana zaidi jinsia ya kike na ndio miongoni mwa
sababu kushindwa kufikia malengo yao.
Wakati
akichangia katika mkutano huo Dkt,Nassra Nassor alisema Kubaguliwa kwa watoto
wa kike katika mambo mengi kwa sababu tu
ya kuwa kwake mwanamke kumekua kukiwadumaza wanawake kiakili na kuwafanya
kudhani wao si sehemu ya jamii wanayopaswa kuwa viongozi badala yake hubaki
nyuma tangu wakiwa wadogo mpaka wanapokua wakubwa.
Alisema
changamoto hizo za kifamilia huwafanya wanawake kuonekana ni wapiti njia mpita njia kwenye familia yake na familia kumuonesha kuwa wao
wanapaswa kusubiri kuolewa tu.
Kwa
upande wake mwanaharakati na mwanasiasa kijana kutokea CHADEMA Zeudi Stephano
alisema haki ya kupata elimu licha ya kuwa ni miongoni mwa haki muhimu za
kikatiba lakinin bado kwenye familia nyingi hadi sasa wamekua wakishindwa kutoa
usawa kwa watoto wakike na wakiume na wapo baadho ya wazazi ambao wamekuwa
wakiwekeza nguvu zao zaidi kwa watoto wa kiume kwenye elimu huku wakiwadumaza
watoto wa kike na kuwafanya wao kutokua sehemu ya watu wanaopaswa kupata elimu
ya kutosha.
Sambamba
na hayo mazingira ya ugawaji wa majukumu kwenye familia nyingi ni sehemu ya
tatizo jengine ambao huwafanya wanawake wengi kushindwa kuwa viongozi kwani
wanawake wengi kwenye familia hupewa majukumu makubwa zaidi kuliko wanaume na
kujikuta muda mwingi wanatumia kufanya kazi baada ya kujisomea.
Nae
Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa
alisema wamebaini kuwa suala la ulizi wa
kupitiliza kwa watoto wa kike limekua likidumaza akili zao na kuwafanya kubaki
na mawazo mgando kutokana na kukosa fursa ya kuchanganyika na wenzao ambapo
tunaamini wangeweza kusoma mambo mapya na ya msingi kwa mustakbali wa maisha
yao.
Hata
hivyo alisema licha ya uwepo wa mazingira ya aina hiyo bado swangependa
kuwakumbusha vijana bado ushiriki wao katika nafasi za uongozi ni muhimu kwa
kuwa ni miomgoni mwa wadau muhimu wa maendeleo na tunapaswa kuendelea kuchukua
juhudi mbalimbali ili kuwezesha ushiriki mpana katika maendeleo ya nchi yetu.
Comments
Post a Comment